Psalms 51:2-7

2 aUnioshe na uovu wangu wote
na unitakase dhambi yangu.

3 bKwa maana ninajua makosa yangu,
na dhambi yangu iko mbele yangu daima.
4 cDhidi yako, wewe peke yako, nimetenda dhambi
na kufanya yaliyo mabaya machoni pako,
ili uthibitike kuwa wa kweli unenapo,
na kuwa na haki utoapo hukumu.
5 dHakika mimi nilizaliwa mwenye dhambi,
mwenye dhambi tangu nilipotungwa mimba kwa mama yangu.
6 eHakika wewe wapendezwa na kweli itokayo moyoni,
ndani sana ya moyo wangu wanifundisha hekima.

7 fNioshe kwa hisopo, nami nitakuwa safi,
unisafishe, nami nitakuwa mweupe kuliko theluji.
Copyright information for SwhNEN